Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahl al-Bayt (a.s) - Abna -; Mtandao wa Al-Mayadeen umeripoti kuwa: Idadi ya Mashahidi wa mashambulizi ya mfululizo ya utawala haram wa Kizayuni katika Ukanda wa Ghaza tangu Jumamosi asubuhi imefikia watu 38.
Mashambulizi haya yanaendelea huku maeneo tofauti ya Ghaza yakilengwa na milipuko mikubwa ya mabomu.
Al Jazeera pia iliripoti dakika chache zilizopita kwamba mtoto ameuawa Shahidi kutokana na shambulio la anga la Israel kwenye nyumba moja Mashariki mwa Khan Yunis Kusini mwa Ukanda wa Ghaza. Pia, Mpalestina mwingine alikufa Shahidi baada ya shambulio la anga la nyumba katika kitongoji cha Jenin, kilichoko Mashariki mwa Mji wa Rafah.
Shirika la habari la Palestina la Shahab limethibitisha kuwa "Salah al-Berdwil" Mjumbe wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Hamas ameuawa Shahidi pamoja na mkewe katika shambulio la mabomu la usiku wa kuamkia leo ya utawala wa Kizayuni huko Magharibi mwa Khan Yunis.
Al-berdwil aliuawa Shahidi wakati akiwa amesujudu katika Sala ya Tahajud akiwa pamoja na mkewe kwenye hema lake katika eneo la al-Nawasi la KhanYunis kutokana na shambulio la anga la adui Mzayuni.
Ikithibitisha kuuawa Shahidi Mwanachama huyo, Harakati ya Hamas imesisitiza kwamba damu ya Shahidi huyo, Mke wake na Mashahidi wote itaendelea kuwa chachu ya vita vya uhuru na kurejea wakimbizi katika nchi yao, na adui hataweza kudhoofisha azma na utulivu wetu.
Your Comment